NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI NA STASHAHADA 2017/2018

  
NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU
NGAZI YA CHETI NA STASHAHADA
KWA VYUO VYA SERIKALI NA VISIVYO VYASERIKALI
KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018
 UTANGULIZI
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatangaza nafasi za mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti Nna Stashahada
kwa mwaka wa masomo
2017/2018.
Masomo yataanza mwezi Septemba, 2017. Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu
Tarajali ambao watapenda kuajiriwa na Serikali
wanapaswa wawe na umri usiozidi miaka 35 wakati
wanapomaliza mafunzo yao. Aidha, waombaji wa mafunzo kazini ambao ni
watumishi wa Serikali na wa mashirika binafsi hawahusiki na umri huu.Kutokana na upungufu
mkubwa wa walimu waSayansi na Hisabati,kipaumbele katika udahili
kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo hayo
.
Wahitimu wa Kidato cha Sita mwaka 2017 wanayo fursa ya kuomba kujiunga na mafunzo ya Stashahada ya Ualimu kwa mwaka2017/2018.Kwa waombaji wa programu za Ualimu katika Vyuo vya Serikali watatakiwa kuomba kupitia tovuti ya  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
 (www.nacte.go.tz) kwa kubofya kwenye Apply online (NOAVS)
kisha kufuata maelekezo.
Kwa waombaji kwenye vyuo visivyo vya Serikali watatakiwa kuomba moja kwa moja kwenye
vyuo husika. Vyuo visivyo vya Serikali vitadahili na kufanya uchaguzi wa wanafunzi wenye sifa na
 kisha kuwasilisha NACTE majina ya waliochaguliwa kwa ajili ya uhakiki
kabla ya kuyatangaza. Vyuo vinaelekezwa kuzingatia utaratibu wa udahili kwa mwaka wa
 masomo 2017/2018 uliotolewa na NACTE.
Maelekezo ya tangazo hili yanawahusu waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya
Serikali na Visivyo vya Serikali.
Kuona vigezo vya kuomba click hii link itakupeleka moja kwa moja kuidanlod hiyo form yao.
http://www.nacte.go.tz/files/ADMISSIONS/NACTE%20Sifa%20za%20kujiunga%20na%20mafunzo%20ya%20Ualimu%20080617.pdf

usisite kutujuza lolote katika blog yako pendwa kwa kuacha comment yako hapa.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA 5 NA UFUNDI 2017

Hatua za kufuata unapotaka fanya application Muhimbili university.

Wanawake wanaopendwa zaid na wanaume