Mambo 7 yanayowaumiza Wanaume Kwenye Mahusiano Kupitia safu yetu ya mahusiano, leo nimekuletea makala maalum hasa kwa wanawake kutokana na malalamiko ya wanawake wengi kuwapoteza waume zao. Kilio chao kikubwa ni kukimbiwa na wanaume au kuachwa. Leo anakuwa na mwanaume huyu, baada ya muda mfupi kunatokea chokochoko, mwanaume anatimka zake. Jamaa anamkimbia na kwenda kuanzisha uhusiano mwingine. Baada ya kukimbiwa, mwanamke hakati tamaa. Anaanzisha uhusiano mwingine, ndani ya muda mfupi tu, anaambulia maumivu tena. Anabaki kujilaumu. Hajui chanzo cha yeye kukimbiwa. Matokeo ya hili, mwanamke anapoteza uelekeo. Kila mwanaume anayekutana naye anamkimbia. Mwisho wa siku anajikuta umri umeenda. Kuolewa inakuwa ni ndoto. Anaanza kulazimisha kusaka mtoto ili angalau na yeye aitwe mama. Wanaume wengi hujikuta wakiwaacha wapenzi wao kwa sababu ya tabia fulani ambazo wakati mwingine huanza taratibu na baadaye huwa kikwazo kikubw...