NA HII NDIO GUIDE BOOK ILIYOTOLEWA NA NACTE KWA PROGRAMS ZA AFYA
HABARINI NDUGU ZANGUNI
Wizara ya afya kupitia NACTE imetoa nafasi za masomo kwa ngazi ya Stashahada na Cheti ambapo imeruhusu ufanywaji wa maombi hayo tokea tarehe 15/05/2017 ambapo wanafunzi wote wanaohitaji soma kozi za afya pitia level hizo tajwa za diploma na certificate wataomba pitia nacte mpaka tarehe 20/08/2017 ndo watafunga kupisha uchaguzi kama tangazo lao lioneshavyo hapa chini
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI WA WANAFUNZI WA ASTASHAHADA NA STASHADA KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)
TAARIFA
KWA UMMA KUHUSU UDAHILI WA WANAFUNZI WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA
KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018
Baraza la
Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa sheria
ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Sura 129, ili kusimamia na
kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini. Sheria hii
inazitaka Taasisi zote zinazotoa elimu ya ufundi kusajiliwa kabla ya
kuanza kuendesha mafunzo yoyote. Baraza pia huidhinisha mitaala kabla
haijaanza kutumika. Hivyo taasisi zote haziruhusiwi kuanza kutoa mafunzo
yoyote bila kibali maalumu kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
(NACTE).
Baraza linapenda kuwataarifu wadau wa sekta ya Mafunzo ya Ufundi na Umma kwa ujumla kuwa udahili na uchaguzi wa wanafunzi kwa ajili ya masomo ya Astashahada na Stashahada mbalimbali yanayotolewa na vyuo vyote hapa nchini, utafanyika moja kwa moja vyuoni,
isipokuwa kozi za afya na ualimu zinazotolewa na vyuo vya Serikali tu.
Hivyo maombi yote ya nafasi za masomo yatumwe kwenye chuo husika.
Udahili
wa kozi za Afya na Ualimu katika vyuo vya Serikali utaratibiwa na
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; na Wizara
ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia kwa kushirikiana na Baraza (NACTE).
Hivyo maombi ya Udahili kwa kozi za Afya na Ualimu kwa vyuo vya serikali tu yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya NACTE au kupitia vyuo husika vya Afya na Ualimu ambavyo vitashughulikia maombi hayo na kufanya udahili kwa njia ya mtandao kupitia ‘Institutional Panel’ zao.
Aidha
vyuo vyote vitatangaza au kuwafahamisha moja kwa moja waombaji majina ya
watakaochaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali; na wale wa kozi za Afya
na Ualimu watatangazwa na Wizara husika na kupitia tovuti ya NACTE.
Baraza
linapenda pia kuwafahamisha kuwa Vyuo vitaanza kupokea maombi ya udahili
wa wanafunzi kuanzia tarehe 15 Mei, 2017 hadi tarehe 20 Agosti, 2017.
Majina ya waliochaguliwa yatatangazwa tarehe 14 Septemba, 2017. Masomo
kwa mwaka wa masomo 2017/2018 yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 25
Septemba, 2017.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 10/05/2017
Na hivi karibuni wametoa guide book yao inayoelekeza vigezo vya anaetaka omba pamoja ada ya chuo husika wameanza toa guide book ya programs za afya alafu wataweka za vyuo vya ualimu kukicheck kitabu hicho bonyeza hiyo link nilokuekea hapa chini utaenda moja kwa moja eneo husika
vilevile kwa wale wanaohitaji ushauri pamoja na kuapply hizi program tuwasiliane pitia 0768445482
Comments
Post a Comment